Breaking

Jumanne, 14 Oktoba 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE: MAN UTD NA CRYSTAL PALACE WAMTAKA BELLINGHAM

 

Manchester United na Crystal Palace wanamfuatilia kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Muingereza Jobe Bellingham, 20. (Bild - in Germany, Subacsription Required)

Arsenal, Manchester City na Real Madrid ni miongoni mwa vilabu vinavyotaka kumsajili beki wa Ujerumani Nathaniel Brown mwenye umri wa miaka 22 kutoka Eintracht Frankfurt, lakini klabu hiyo ya Bundesliga haitasikiliza ofa hadi msimu ujao wa joto. (Bild - in Germany)

Iwapo Eintracht Frankfurt itamruhusu Brown - ambaye hana kipengele cha kutolewa katika mkataba wake - kuhama, klabu hiyo ya Ujerumani itadai pauni milioni 52. (Florian Plettenberg)


Msako wa Chelsea kumnasa Adam Wharton wa Crystal Palace umeongezeka lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester United kumnunua kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 21. (Teamtalks)


#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni: