Breaking

Jumatano, 15 Oktoba 2025

UWANJA WA UHURU WAFIKA ASILIMIA 90 YA MAREKEBISHO

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa amefanya ziara ya kukagua  Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, ambao umefikia asilimia 90 ya ukarabati.

Amefanya ziara hiyo Oktoba 13, 2025 akiwa ameongozana na  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndg. Methusela Ntonda ambapo ukamilishaji huo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kuboresha miundombinu ya michezo nchini.

"Serikali inaendelea kusimamia kwa karibu ukarabati huo ili kuhakikisha viwango vya kimataifa vinazingatiwa na lengo ni kuona uwanja huu  unarejea katika hadhi yake" alisema Msigwa.

Kati ya maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ni pamoja na ufungaji wa taa mpya za kisasa, uwekaji wa nyasi bora za bandia (Pitch), Paa la uwanja marekebisho ya njia za kukimbilia (Running Track), ufungaji wa viti vipya, ukarabati wa vyoo, ufungaji wa milango mipya na uwekaji wa vigae vipya pembezoni mwa uwanja.




Ukarabati wa Uwanja wa Uhuru ni sehemu ya mipango ya serikali wa kuboresha viwanja vya michezo nchini ikiwa ni utekelezaji wa Serikali ya Awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kufanya michezo kuwa nyezo ya ajira na uchumi.

#Official-Isharoja✍🏾

Hakuna maoni: