Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), tarehe 11 Oktoba 2025 katika Wilaya ya Momba, Kata ya Kamsamba, Mkoani Songwe. Ameinadi Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, Huku akiwaomba Wananchi Kukichagua Chama Cha Mapinduzi ifikapo oktoba 29,2025.
Pamoja na mambo mengine Chatanda kupitia Mkutano huo wa Kampeni, amemuombea Kura za Heshima Mgombea wa Nafasi ya Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Momba, Ndg. Condester Sichalwe na Madiwani wa Kata kwa tiketi ya CCM, kupitia Jimbo hilo sambamba na hilo Wananchi wa Momba wamemuahidi Chatanda kuwa Watapiga Kura za Kishindo kwa Wagombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM ili kuitimiza furaha yao kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.









Hakuna maoni:
Chapisha Maoni