Breaking

Jumanne, 9 Desemba 2025

LIVERPOOL NA MAN CITY ZAMMEZEA MACHO DIOMANDE

 


Klabu mbili kongwe za Ligi Kuu England, Liverpool na Manchester City, zimeripotiwa kuingia vitani kumnasa beki wa Sporting CP, Ousmane Diomande, ambaye amekuwa akikiongoza safu ya ulinzi ya klabu hiyo ya Ureno kwa kiwango cha juu katika misimu ya hivi karibuni.


Diomande, mwenye umri wa miaka 20, ameendelea kuvutia mashabiki na makocha barani Ulaya kutokana na uwezo wake wa kukaba kwa utulivu, kujenga mashambulizi kutoka nyuma, pamoja na kasi inayomfanya kuwa beki wa kisasa anayewafaa timu za presha ya juu kama Liverpool na Man City.


Ripoti zinadai kuwa Sporting CP inaweza kuanza mazungumzo kwa dau linalokadiriwa kufikia zaidi ya €60 milioni, kiasi ambacho kinaonyesha thamani na umuhimu wa mchezaji huyo katika kikosi chao.


Kwa upande wa Liverpool, kocha wao anadaiwa kutaka kuongeza chaguo sahihi la ziada kwenye eneo la ulinzi kufuatia majeraha ya mara kwa mara yanayowakumba baadhi ya wachezaji wake.

Man City nao hawako nyuma, wakihitaji kuongeza kina kwenye safu yao ya ulinzi kutokana na ratiba ngumu inayoambatana na mashindano mengi.


Hadi sasa hakuna klabu iliyowasilisha ofa rasmi, lakini wadadisi wa soka Ulaya wanaamini kuwa mchuano wa kumpata Diomande unaweza kuwa miongoni mwa “vita” kubwa za usajili katika dirisha lijalo.


Matarajio ni kwamba tetesi hizi zitaongezeka kadri dirisha la usajili linavyozidi kukaribia, huku mashabiki wakisubiri kuona ni klabu ipi itafanya hatua ya kwanza kumtwaa beki huyo chipukizi mwenye kipaji kikubwa.


Hakuna maoni: