Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wapya wa Bodi za Wakurugenzi katika taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), uteuzi unaolenga kuimarisha ufanisi wa uendeshaji wa taasisi hizo.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, walioteuliwa ni kama ifuatavyo:
Ndugu Makame Hasnuu Makame ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri Zanzibar (ZMA). Ndugu Makame ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Meli na Uwakala Zanzibar (SHIPCO).
Ndugu Sultan Said Suleiman ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO). Ndugu Sultan kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC).
Ndugu Juma Burhan Mohamed ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA). Ndugu Juma ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA).
Dkt. Maudline Cyrus Castico ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA). Dkt. Maudline ni Waziri Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Aidha, Dkt. Idrissa Muslim Hija ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Karakana Zanzibar, ambapo ni Katibu Mkuu Mstaafu wa SMZ.
Uteuzi wa viongozi hao unaanza rasmi tarehe 22 Disemba, 2025.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni