Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo, amewakikishia wakazi wa kata ya kitunda na kata jirani kukamilika kwa ujenzi wa shule ya sekandari ya kitunda relini kabla ya muda wa mkataba wa ujenzi huo.
Ametoa kauli iyo wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Reuben Kwagilwa, alipofanya ziara ya siku moja wilayani Ilala, katika jimbo la Kivule kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya elimu na miundombinu ya barabara.
Mkuu huyo wa wilaya ya ilala, Edward Mlogolo, amebainisha kuwa ujenzi huo ulianza mwezi Septemba 2024 kwa mkataba wa muda wa miezi 18 lakini hadi kufikia sasa mradi huu umefika zaidi ya asilimia 96.
Huku akitumia nafasi hiyo, kumshukuru sana Rais Dokta Samia Suluhu Hassan, kwa uwezeshaji huo na viongizi wanaamini mradi umetekelezwa ndani ya mwaka mmoja na wanathibitisha matumizi mazuri ya muda na thamani ya walipa kodi za Watanzania.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni