Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, mwingi wa rehema, kwa kumjalia uhai na kumfikisha salama katika siku ya kumbukizi ya kuzaliwa, akitimiza umri wa miaka 66.
Kupitia ujumbe wake, Rais Samia ameonesha shukrani za dhati kwa Watanzania na wadau mbalimbali waliomfikishia salamu, pongezi na dua za upendo katika siku hiyo muhimu. Amesema amezipokea salamu hizo kwa moyo wa furaha na unyenyekevu, akisisitiza kuwa upendo huo unaendelea kumpa nguvu ya kuwatumikia Watanzania kwa bidii na kujitolea.
Katika kuadhimisha kumbukizi hiyo, Rais Samia ameamua kusherehekea kwa vitendo vyenye manufaa kwa taifa na vizazi vijavyo, kwa kushiriki zoezi la kupanda miti kama ishara ya shukrani kwa uhai na dhamira ya kulinda mazingira.
Aidha, Rais Samia ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kujenga na kuimarisha utamaduni wa kupanda miti na kutunza mazingira, akisisitiza kuwa mazingira yakilindwa leo, yataendelea kuwalinda wananchi na vizazi vijavyo. Amesema juhudi za pamoja katika uhifadhi wa mazingira ni msingi muhimu wa maendeleo endelevu ya taifa.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni