Breaking


Jumanne, 20 Januari 2026

SEMINA YA MAFUNZO ELEKEZI KUHUSU SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI YAKAMILIKA

Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Taasisi zilizopo chini yake imehitimisha Semina ya Mafunzo Elekezi iliyotolewa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo kuhusu shughuli zinazo ratibiwa na kusimamiwa na Wizara hiyo.

Akizungumza kwenye tamati ya semina, Mwenyekiti  wa Kamati hiyo Mhe. Deudatus Mwanyika aliwapongeza viongozi pamoja na wataalam wa wizara hiyo kwa uwasilishaji mzuri wa semina hiyo ya siku 2 iliyoanza Januari 19, 2026 na kuhitimishwa leo Januari 20, 2026 Bungeni Jijini Dodoma.

Aidha Mhe. Mwanyika amesisitiza wizara kuendelea kuboresha matumizi ya teknolojia za kisasa za kitafiti pamoja na mafunzo yanayoendana na teknolojia hiyo kwa watumishi na wataalamu wa sekta zote ili kuongeza thamani ya mazao ya mifugo na uvuvi.

Akitolea ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wajumbe wa kamati hiyo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema Wizara yake inaendelea kuimarisha na kuboresha huduma zinazotolewa na sekta hizo na kuahidi ushirikiano wa dhati na kamati hiyo. 

Aidha aliongeza kuwa yapo mabadiliko mengi yanayoendelea kwenye sekta hiyo yanayolenga kutatua changamoto za wananchi pamoja na wadau wa sekta hiyo ya mifugo na uvuvi.

Semina hiyo ililenga kuliongezea Bunge uelewa kuhusu sekta ya Mifugo na Uvuvi na mabadiliko yanayotarajiwa katika sekta hiyo.

Hakuna maoni: