Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, amewasili mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo katika sekta ya afya pamoja na kujionea hali ya utolewaji wa huduma kwa wananchi.
Akiwasili leo Machi 04, 2026, amepokelewa na Mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa, ambapo ziara hiyo inalenga kuimarisha usimamizi, kuongeza ufanisi wa huduma na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya afya kwa manufaa ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya.
Katika ziara hiyo, Dkt. Samizi pia asisitiza utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote ili kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora bila changamoto za kifedha, pamoja na kuimarisha mfumo wa kupokea mrejesho (feedback) kutoka kwa wagonjwa baada ya kupata huduma hatua ambayo inalenga kuongeza uwajibikaji, kubaini maeneo ya maboresho na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakidhi matarajio na viwango vya ubora vinavyotakiwa.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni