Katibu wa NEC Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa (CCM) Kenan Kihongosi amesema matumizi ya teknolojia ya kisasa ya ndege nyuki katika kunyunyuzia dawa na kuangamiza wadudu waharibifu yamechangia kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la Pamba Mkoani Simiyu kutoka wastani wa kilo 200 hadi kufikia kilo 1000 kwa ekari.
Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo unaolenga kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao na kuboresha kipato chao.
Baadhi ya wakulima wa kijiji cha Mwatumbe, Kata ya Shishiyu Wilayani Maswa wamesema matumizi ya teknolojia hiyo yamepunguza gharama na muda wa kunyunyuzia dawa mashambani huku yakisaidia kudhibiti wadudu waharibifu kwa ufanisi zaidi.
Wakulima hao wamesema ongezeko la uzalishaji linawapa matumaini ya kupata mavuno mengi zaidi na kuongeza kipato cha familia zao.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni