Breaking


Jumatatu, 13 Aprili 2026

KIM KARDASHIAN NA LEWIS HAMILTON WAIBUA GUMZO BAADA YA KUONEKANA PAMOJA COACHELLA

 

Mastaa wawili wakubwa duniani, Kim Kardashian na Lewis Hamilton, waliibua gumzo mitandaoni baada ya kuonekana pamoja kwa staili ya kimya kimya jangwani kwenye tamasha la Coachella

Wawili hao walifanya “low-key link-up” iliyowashangaza wengi, wakionekana wakifurahia mazingira ya kipekee ya tamasha hilo maarufu duniani bila makelele mengi ya umaarufu wao.

Mashabiki na wapiga picha walinaswa wakijaribu kunasa matukio yao, huku picha na video chache zikianza kusambaa zikionesha wawili hao wakizungumza kwa ukaribu na kuonekana kufurahia muda wao pamoja.

 Ingawa hakuna aliyetoa maelezo rasmi kuhusu kilichowaunganisha katika tukio hilo, uwepo wao umechochea mjadala mkubwa mtandaoni, wengi wakijiuliza kama ni urafiki wa kawaida au kuna kitu zaidi kinaendelea nyuma ya pazia.


Coachella imeendelea kuwa sehemu ya kukutana mastaa wakubwa wa burudani na michezo, lakini muonekano huu wa ghafla wa Kim na Hamilton umeongeza ladha ya kipekee mwaka huu. 

Kwa sasa, mashabiki wanaendelea kufuatilia kwa karibu kila ishara mpya, wakisubiri kuona kama huu ulikuwa mwanzo wa urafiki mpya au tukio la muda tu lililobeba headline kubwa.


Hakuna maoni: