Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa mtandaoni, baadhi ya mashabiki wameonyesha kutoridhishwa na matokeo ya haraka tangu kuwasili kwa Mbappé ndani ya kikosi hicho, wakiamini kuwa bado hajaonesha kiwango walichokuwa wakikitarajia baada ya kujiunga na miamba hiyo ya soka barani Ulaya.
Aidha, baadhi ya wachambuzi wa soka wanaeleza kuwa mjadala huo umechangiwa pia na mabadiliko ya mfumo wa timu pamoja na namna anavyotumika uwanjani, jambo ambalo limezua maoni tofauti miongoni mwa wapenzi wa klabu hiyo.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na Real Madrid wala Mbappé mwenyewe kuhusu ombi hilo la mtandaoni, huku wengi wakiamini kuwa ni sehemu ya hisia za mashabiki zinazotokana na presha ya mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo.
Wakati mjadala ukiendelea mjini Madrid na kwenye majukwaa mbalimbali ya michezo, baadhi ya mashabiki wameendelea kumtetea Mbappé wakisisitiza kuwa nyota huyo anahitaji muda zaidi kuzoea mfumo wa timu pamoja na ushindani wa ligi ya La Liga.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni