Breaking


Jumatano, 13 Mei 2026

TRUMP AANZA ZIARA YAKE RASMI YA CHINA

Rais wa Marekani, Donald Trump, anatarajiwa kuwasili mjini Beijing kwa ziara ya kwanza ya China kwa Rais wa Marekani katika kipindi cha karibu mwongo mmoja.

Rais Trump aliondoka Washington jana na akasema anatarajia mazungumzo "marefu" na Rais Xi Jinping, kuhusiana na Iran, ambayo inaitegemea China kama mteja wake mkuu wa mafuta yake yaliyowekewa vikwazo na Marekani.

Kiongozi huyo wa Marekani lakini amesema hatohitaji usaidizi wowote wa China kwa Iran.

Rais Trump amesema pia kuwa atazungumza na Rais Xi kuhusu Marekani kuiuzia silaha Taiwan, kisiwa chenye utawala wa ndani ambacho China inadai kuwa ni sehemu ya himaya yake.

Hatua hii itakuwa ni kinyume cha utamaduni wa kihistoria wa Marekani wa kutojadiliana na China kuhusiana na kukiunga mkono kisiwa hicho.

Wakuu hao wa nchi mbili zenye uchumi mkubwa zaidi duniani pia wanatarajiwa kujadiliana kuhusu uhusiano wao wa kibiashara na udhibiti wa China wa uuzaji wa madini muhimu yaliyo nadra.

Hakuna maoni: