Simba imemtambulisha kiungo mkabaji, Alassane Kante raia wa Senegal akitokea CA Bizertin ya Tunisia kwa mkataba wa miaka miwili.
Kante anatarajiwa kuongeza nguvu kubwa katika kikosi cha Simba baada ya kuonyesha kiwango kizuri akiwa na CA Bizertin.
Kiungo huyo atakuwa Msimbazi hadi 2027 huku mkataba wake ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni