Breaking


Jumanne, 29 Julai 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA : EVERTON INAMFUKUZIA GREALISH MAN CITY

 

picha, Mchezaji wa Man City Jack Grealish akiwa na Kocha Pep Guardiola

Everton ina nia ya kumsajili kiungo wa Uingereza Jack Grealish, 29, kwa mkopo lakini inakabiliwa na ushindani kutoka kwa West Ham na Napoli. (ipaper - usajili unahitajika)

Alexander Isak, 25, ameidhinisha masharti ya kibinafsi na Liverpool kwa kandarasi ya miaka mitano ikiwa ada itakubaliwa kumsaini mshambuliaji huyo wa Newcastle na Uswidi. (Sky Sports Uswisi - kwa Kifaransa)

Brentford haiko tayari kumtoa mshambuliaji wa DR Congo Yoane Wissa, 28, kwa Newcastle kwa bei yoyote isipokuwa wasajili kwanza mbadala wake. (ipaper - usajili unahitajika)

#Chanzobbcswahili

Hakuna maoni: