Liverpool inatarajiwa kumenyana na Newcastle United katika kinyang'anyiro cha mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Mfaransa Hugo Ekitike, 23, baada ya kufahamishwa kuwa mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, hatahama klabu yake katika dirisha hili la usajili. (Sky Sports)
The Magpies inahisi kuvujishwa kwa ofa ya Liverpool ya pauni milioni 120 kulilenga kumtatiza Isak. (Telegraph - usajili unahitajika)
Pamoja na Ekitike, Liverpool pia inawafukuzia washambuliaji wengine wanne endapo itamkosa Isak - wachezaji hao ni pamoja na Ollie Watkins wa Aston Villa, 29, Victor Osimhen wa Napoli, 26, Yoane Wissa wa Brentford, 28, na Rodrygo wa Real Madrid, 24. (Mail+ - usajili unahitajika)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni