Breaking

Jumatano, 23 Julai 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA:RODRYGO KUMRITHI LUIS DIAZ LIVERPOOL ?

Winga wa Real Madrid na Brazil Rodrygo, 24, ni mmoja wa nyota wa kumrithi Luis Diaz huko Liverpool iwapo winga huyo wa Colombia mwenye umri wa miaka 28 ataondoka Anfield (Florian Plettenberg).

Mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 25, anataka pauni 300,000 kwa wiki kusaini mkataba mpya Newcastle (Talksport).

Granit Xhaka amekubaliana masharti na Sunderland, huku klabu hiyo sasa ikiwa kwenye mazungumzo na Bayer Leverkusen kuhusu ada ya kiungo huyo wa Uswisi mwenye umri wa miaka 32 (Times). 

Atalanta na Lazio wanavutiwa na mshambuliaji wa Manchester United na Denmark Rasmus Hojlund, 22 (Footmercato).

Atletico Madrid wameanza mazungumzo na Chelsea kuhusu mpango wa kumsajili Renato Veiga, huku Blues wakidai takriban pauni milioni 35 kumuachia beki huyo wa kati wa Ureno mwenye umri wa miaka 21 (Fabrizio Romano).

Hakuna maoni: