MGOMBEA wa nafasi ya Rais kwa tiketi ya Chama Cha Ada Tadea,Georges Bussungu,amechukua fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya urais na kutoa pole kwa Chama Cha Mapinduzi(CCM),na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumpoteza Spika Mstaafu Job Ndugai.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 11,2025,mara baada ya kuchukua fomu katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC),zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma,Bussungu akiwa ameambatana na mgombea mwenza wake Ali Makame Issa amesema chama kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo chake.
“Kwanza nianze kutoa pole kwa Bunge na CCM,kwa msiba mzito uliotokea wa Hayati Ndugai,sisi kama chama tunasikitika sana kwa kifo hicho na tunatoa pole kwa familia yake,”amesema.
Bussungu amesema mtazamo wa chama chake ni kuleta makubwa katika jamii ya fikra,teknolojia na uchumi kwa kuzingatia kuwa ulimwengu wa sasa umebadilika ni wa akili mnemba .




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni