Breaking


Jumatatu, 11 Agosti 2025

UMD YAJA NA SERA ZA MAJIMBO.

MWAJUMA Milambo kutoka chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD),amekuwa mwanamke wa pili kuchukua fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu Agosti 9,2025.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 11,2025,mara baada ya kuchukua fomu katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC),Mwajuma aliyeambatana na mgombea mwenza Mashavu Alawi Haji amesema UMD ipo tayari kuanza harakati za kusaka dola ikiwa ni hatua muhimu ya kutimiza takwa la kikatiba.

"UMD tupo tayari kuanza harakati za uchaguzi, tunaamini kupitia sera wezeshi zenye kumgusa kila Mtanzania,Chama chetu kinaamini katika sera za majimbo zenye kumnufaisha mwananchi kufurahia fursa za kiuchumi zilizopo eneo lake na Taifa kwa ujumla," amesema.

Hakuna maoni: