Breaking


Jumanne, 26 Agosti 2025

BOTSWANA YATANGAZA HALI YA DHARURA KUFUATIA UHABA WA DAWA

Botswana imetangaza hali ya dharura ya kiafya kufuatia kuporomoka kwa mnyororo wake wa usambazaji wa bidhaa za matibabu.

Rais Duma Boko wa Botswana amelihutubia taifa akisema hospitali nyingi nchini humo zina uhaba wa dawa muhimu.

Tayari Wizara ya Fedha imeidhinisha bajeti ya dharura ya dola Milioni-18.7 ili kuushughulikia mzozo huo. 

Rais Duma Boko alisema jeshi litasimamia usambazaji wa dawa za dharura, huku shehena za kwanza zikiondoka mara moja katika Mji Mkuu wa Gaborone na kuyapa kipaumbele maeneo ya vijijini ambayo hayajahudumiwa.

Tangu kuanza kwa mwezi huu, Wizara ya Afya ilikuwa imeziagiza hospitali kuahirisha shughuli zisizo za lazima kwa sababu ya uhaba wa dawa. 

Botswana ni miongoni mwa mataifa kadhaa barani Afrika yaliyoathiriwa na hatua ya hivi karibuni ya serikali ya Marekani kupunguza misaada ya maendeleo katika sekta ya afya. 

Mgogoro huo pia unahusishwa na kupungua kwa bajeti ya taifa kulikosababishwa na kudorora kwa soko la Almasi Duniani. 

Botswana yenye wakazi Milioni-2.5 Kusini mwa Afrika ni mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa Almasi Duniani.

#ChanzoDWSwahili

Hakuna maoni: