Breaking


Jumanne, 12 Agosti 2025

CCK YACHUKUA FOMU INEC

 

Mgombea urais kupitia Chama cha kijamii (CCK) David Mwaijojele amesema moja ya vipaumbele vyake vikuu ni kuhakikisha wastaafu wanapata maisha bora baada ya kustaafu pamoja na kuendeleza kilimo cha kisasa..

Mwaijojele amesema hayo Agosti,12,2025, mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba nafasi ya Urais katika Ofisi za Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), zilizopo jijini Dodoma akiwa ameambatana na mgombea mwenza Masoud Ali Abdallah.

Amesema Sera za Chama chake zitalenga kuweka mazingira sahihi kwa wastaafu kuishi kwa heshima na kupata usaidizi katika changamoto wanazokumbana nazo..

Aidha, amesisitiza kuboresha elimu kwa kuongeza ubora wa mitaala na Mazingira bora kwa walimu.

Hakuna maoni: