Katika tukio kubwa la kihistoria linalofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Tanzania imeandika ukurasa mpya katika historia ya soka barani Afrika kwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa yenye hadhi kubwa.
Kwa upande wake Kocha Mkuu wa timu ya taifa, Hemed Suleiman maarufu kama ‘Morocco’, Amesema mashindano haya hayawakilishi tu heshima ya kuwa wenyeji.
Kwa mtazamo wake, tukio hili ni zaidi ya mechi za dakika tisini ni mwanzo mpya wa safari ya kisoka la Tanzania.
Kocha Morocco amesisitiza kuwa tukio hili ni fursa kwa vijana wengi kuhamasika, kwa wachezaji kuonesha vipaji vyao mbele ya macho ya dunia, na kwa taifa zima kutambua thamani ya kuwekeza katika michezo.
Mashindano haya yameleta pamoja mataifa mbalimbali, yakionesha si tu ushindani wa kiuchezaji bali pia mshikamano wa kitamaduni na kiurafiki, hali ambayo imelitangaza taifa la Tanzania kama mwenyeji mwenye ukarimu na maandalizi ya kiwango cha juu.
Mashabiki, viongozi wa michezo, na wadau mbalimbali wamepongeza kauli ya Kocha Morocco, wakisema kuwa maneno yake yanaakisi ari mpya inayotakiwa kuendelea kujengwa kwa ajili ya kizazi kijacho cha soka.
Madelemo News itaendelea kukuletea taarifa zote muhimu kuhusu mashindano haya, matokeo ya mechi, mahojiano ya kipekee, na taswira kamili ya jinsi Tanzania inavyoandika historia mpya kwenye ulimwengu wa michezo.
Chanzo: TFF | MichuanoLive2025 | Madelemo News ripoti ya uwanjani.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni