Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg. Gerson Msigwa amepokea tiketi 10,000 za mashabiki kuishangilia Taifa Stars dhidi ya Madagascar kutoka Benki ya CRDB.wakiunga mkono Serikali iliyotoa tiketi elfu 10 za mchezo utakaochezwa leo Agosti 9, 2025 katika
Uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 2 usiku.
Msigwa amepokea tiketi hizo mapema leo mbele ya wanahabari kwa kukabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 20 na Mkuu wa kitengo cha Masoko, Bi. Joseline Kamuhanda huku akiwataka watanzania kufika kwenye matawi ya CRDB jijini Dar es Salaam kuchukua tiketi hizo.
Vituo vya CRDB vya Dar es salaam vitakavyotoa tiketi hizo ni Temeke, Mbagala, Buza, Tandika, Banana, Gongolamboto, Mbande, Ubungo, matawi ya Kariakoo, Posta pamoja na Kinyerezi.
Mashabiki wa Tanzania wana tiketi elfu 20 za bure kuingia na kuishangilia Mechi ya Taifa Star dhidi Madagascar leo Agosti 09, 2025 ndani ya dimba la Benjamin Mkapa Dar es salaam.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni