MGOMBEA urais wa Chama Cha Democratic Party(DP),Abdul Mluya,amechukua rasmi fomu ya kugombea nafasi hiyo huku akiahidi kuwa serikali yake itawajibika kuwatunza mama wajawazito na watoto kwa kipindi cha miezi mitatu baada ya kuzaliwa.
Mluya amechukua fomu hiyo leo katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC),Jijini Dodoma akiwa ameambatana na mgombea mwenza wake Sadous Abrahman khatib ambapo amesema huduma hiyo ya bima ya afya bure itaambatana na huduma zote za lishe.
Aidha,ameahidi kuimarisha huduma za mama wajawazito ili kuhakikisha afya ya mama na mtoyo inalindwa kikamilifu.
Kwenye upande wa sekta ya kilimo ameaahidi kukifanya kiwe endelevu kwa kuondoa jembe la mkono ili waweze kulima kisasa na hivyo kupata mazao yenye tija yatakayouzwa nje na kuwezesha Taifa kupata fedha za kigeni.
Chama cha DP kimekuwa cha 12 kati ya vyama 18 vivilivyothibitisha kufika Ofisi za INEC kwa ajili ya kuchukua fomu za uteuzi kwa wanachama wa vyama vya siasa waliopendekezwa kugombea kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni