Breaking


Jumamosi, 16 Agosti 2025

KADOO KUENDELEA KUKUZA UCHUMI WA NCHI KWA KUTOA AJIRA KWA WATANZANIA

Zaidi ya ajira 80 zimepatikana katika uwekezaji wa kampuni ya kubadilisha fedha ya Kadoo katika mikoa 27 nchini Tanzania.

Hii ni kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Kadoo Bureau De Change upande wa Ulinzi, Justine Amos.

Amosi alikuwa akizungumza katika uzinduzi wa maduka mawili kwa mpigo ya kubadilisha fedha ya Kadoo, moja likiwa Ubungo jingine likiwa ndani ya Dar Village Mall jijini Dar es salaam.

Aidha, Kadoo Bureau De Change umeipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji yanayochochea wawekezaji wengi kuja kuwekeza nchini Tanzania, hatua inayochochea uwepo pia wa maduka ya kubadilisha fedha kwa ajili ya wageni na watanzania kwa ujumla ili kukidhi takwa la matumizi ya shilingi nchini.

Hakuna maoni: