Breaking


Jumapili, 31 Agosti 2025

MIAKA MITANO IJAYO TUTANUNUA TREKTA MILIONI 10- RAIS SAMIA

MGOMBEA Urais kupitia Chama ChaMapinduzi(CCM),Rais Dokta Samia Suluhu Hassan,amesema serikali itakaporudi madarakani  itanunua Trekta milioni 10 katika kipindi cha miaka mitano ijayo ahadi inayodhihirisha utayari wa kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo nchini.

Mkakati huo utaambatana na ununuzi wa zana zingine za kilimo ambazo zitasambazwa katika kanda maalum kwa lengo la kumrahisishia mkulima kupata mazao bora ya chakula na biashara.

Rais Dokta Samia amesema hayo leo wakati akizungumza na wananchi  katika mkutano wa kampeni Chemba ambapo amesema Trekta hizo zitakodishwa kwa wakulima nusu ya bei watakayotozwa na watu binafsi wanapolimiwa kwa kila ekari moja.

Lengo la kufanya hivyo ni kumpunguzia mkulima adha ya kukodi vifaa na zana za kilimo kwa watu binafsi ambao kwa ekari moja wanalimiwa hadi shilingi 80,000 ambazo wamenza kushusha kufikia shilingi 40,000 baada ya serikali kuanza kuweka vituo hivyo.

Hakuna maoni: