DAHANE BEIDA @dahane2006 refa wa kimataifa mwenye Beji ya FIFA toka nchini @ffrim ameteuliwa kuwa Refa wa VAR katika mchezo wa kesho Tanzania vs Morocco katika michuano ya CHAN @caf_online inayoendelea.
Huyu Refa ni Muuaji katika maamuzi yake ndani ya mpira kwa Watanzania na historia inajua hivyo na hapendwi wala kutakiwa kuwepo katika michezo ya Tanzania maana tayari nyongo zimetumbuka juu yake.
Mechi ya Mamelod vs Yanga alituuua waziwazi kule South Africa katika CAF Champions league ila tukio la hivi karibuni ni la Fainali ya CAF Confederation Cup kule Zanzibar Simba vs Berkane toka Morocco alitoa maamuzi anayojua yeye na kuacha vidonda sana kwa Tanzania baada ya ile mechi hakuweza kuondoka na ndege alikuja nayo bali ndege binafsi iliyoandaliwa na Rais wa Soka la Morocco na Makam wa Rais wa CAF bwana Ferouz Lekjaa @tft_morocco hii ni kuonyesha ni refa wa Mipango anaelindwa na @caf_online
Sasa Katika mchezo ambao Tanzania inacheza dhidi ya Taifa la Morocco ameletwa tena yule Refa wa Mipango na kusimamia VAR hii ni dhairi kuonyesha kuna Mipango inasukwa na Watanzania safari hii Hatutakubali
#ChanzoJemedarisaid

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni