Breaking


Jumanne, 19 Agosti 2025

NMB YACHANGIA MILIONI 30 KUIUNGA MKONO TAIFA STARS KWENYE SAFARI YA CHAN

 

Kombe linakuja nyumbani!

Kama mdau wa michezo nchini, tumeungana na Baraza la Michezo la Taifa chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuiunga mkono Taifa Stars ambayo imefuzu kwenda robo fainali ya mashindano ya CHAN, ikiwa ni mara ya kwanza.


Tumewasilisha mchango wa jumla ya Tsh milioni 30, ambapo milioni 20 inaenda kuchangia tiketi 10,000 kwenda kuangalia mechi dhidi ya Morocco, na milioni 10 ni motisha kuipa nguvu timu yetu kuendelea kujituma zaidi.

Mchango huu umepokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, na uwakilishi wa benki umeongozwa na Mkuu wetu wa Idara ya Mauzo na Mtandao wa Matawi, Donatus Richard.


#NMBKaribuYako

Hakuna maoni: