Breaking


Jumapili, 31 Agosti 2025

PPPC YASISITIZA USHIRIKIANO WA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI


Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), David Kafulila amewataka Watanzania kutumia kikamilifu fursa za kimaendeleo zilizopo nchini ili kuinua kipato chao na kukuza uchumi wa taifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mdahalo wa kiuchumi ulioandaliwa na PPPC na kuhudhuriwa na wachambuzi wa masuala ya uchumi, Kafulila amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki zilizo na rasilimali nyingi na muhimu ambazo zikitumika vizuri zinaweza kubadilisha maisha ya wananchi.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na sekta ya umma katika kutekeleza miradi ya kimkakati, akibainisha kuwa njia hiyo ndiyo chachu ya kuharakisha maendeleo na kutengeneza ajira kwa vijana.

Hakuna maoni: