Breaking


Jumanne, 12 Agosti 2025

RAIS SAMIA AZINDUA HARAMBEE YA CCM YA KUCHANGISHA SHILINGI BILIONI 100 ZA KAMPENI

 



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan, amezindua zoezi la Harambee ya chama hicho iliyolenga kuchangisha fedha za kusaidia Kampeni za CCM, ambapo naye amechangia Shilingi Milioni Mia 1.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Harambee hiyo usiku huu katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es salaam, Rais Dokta Samia amewaomba wana CCM wachangie kwa maendeleo ya CCM na pia CCM  iweze kwenda kwa wananchi kunadi Sera zake.

Awali Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dokta Emmanuel Nchimbi, amesema msingi wa Harambee hiyo ni maombi ya wana CCM ambao wanataka kuchangia maendeleo ya chama Chao.Katika Harambee hiyo, CCM imedhamiria kukusanya Shilingi Bilioni mia 1.

Hakuna maoni: