Breaking


Ijumaa, 1 Agosti 2025

RAIS SAMIA AZINDUA KITUO CHA BIASHARA NA USAFIRISHAJI AFRIKA MASHARIKI (EACLC) UBUNGO, DAR ES SALAAM

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 01, 2025, amewasili na kushiriki katika tukio la kihistoria la uzinduzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Afrika Mashariki (East Africa Commercial and Logistics Centre – EACLC) kilichopo eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo muhimu, Mhe. Rais alipata fursa ya kushuhudia maendeleo ya miundombinu ya kisasa inayolenga kuimarisha biashara za kikanda na usafirishaji barani Afrika. Kituo hiki kinatarajiwa kuwa kiunganishi muhimu kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kikichochea kasi ya ukuaji wa uchumi na ushirikiano wa kibiashara.


Fuata picha na matukio mbalimbali ya uzinduzi huo kupitia Madelemo News.


Hakuna maoni: