Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chilya, amewataka watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto mkoani humo kuongeza juhudi katika utoaji elimu kwa jamii juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji.
Akizungumza na watendaji hao, Kamanda Chilya amesema ni muhimu kuimarisha mahusiano mazuri na jamii zinazowazunguka ili kupata taarifa za uhalifu mapema na kuzuia madhara makubwa yanayoweza kuwapata wahanga.
“Fanyeni kazi kwa weledi, haki na uadilifu. Wahudumieni waathirika wa ukatili kwa heshima, na tunzeni siri za wale wote wanaotoa taarifa. Hii itajenga imani kubwa kati yenu na jamii,”
SACP Marco G. Chilya
Kwa upande wake, Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Ruvuma, ASP Odilia Mroso, amesema ataendelea kusimamia mipango ya utoaji elimu kwa watendaji wa dawati katika kila wilaya ili kupunguza vitendo vya ukatili na uhalifu vinavyotokana navyo.
🌍 Ruvuma inasema hapana kwa ukatili wa kijinsia!
👩👧👦 Elimu, ushirikiano na uadilifu ndio silaha ya kulinda familia na watoto.
#Ruvuma #UsalamaKwanza #PingaUkatili #JeshiLaPolisi #ElimuKwaJamii #UkatiliWaKijinsia

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni