Breaking


Jumamosi, 23 Agosti 2025

SENEGAL YATINGA NUSU FAINALI YA CHAN 2024 BAADA YA KUICHAPA UGANDA



Timu ya taifa ya Senegal imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Michuano ya CHAN 2024 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uganda katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Kampala.


Bao pekee la mchezo huo lilitosha kuipa Senegal tiketi ya kusonga mbele na kuendeleza rekodi nzuri kwenye mashindano hayo ya mataifa ya wachezaji wa ndani barani Afrika.


Kwa kipigo hicho, Uganda imeungana na Kenya na Tanzania (ambao ndio wenyeji wa mashindano haya) kuaga michuano hiyo, licha ya jitihada zao za kutafuta nafasi ya kusonga mbele kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki.


🔚 Matokeo ya Mwisho:

🇺🇬 Uganda 0 – 1 Senegal 🇸🇳


Senegal sasa itasubiri kufahamu mpinzani wake katika hatua ya nusu fainali itakayochezwa mwishoni mwa wiki ijayo.


NUSU FAINALI YA CHAN 2024


Mechi

Timu

Uwanja

Tarehe

Nusu Fainali 1

Senegal 🇸🇳 vs ???

Nelson Mandela Stadium, Kampala

Kutangazwa

Nusu Fainali 2

??? vs ???

Benjamin Mkapa Stadium, Dar es Salaam

Kutangazwa


Hakuna maoni: