Shirika la Reli Tanzania (TRC) linautahadharisha umma kuhusiana na tabia iliyojitokeza hivi karibuni ya baadhi ya watu kujihusisha na utoaji wa tiketi za huduma ya reli ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) kinyume na utaratibu.
Shirika linapenda kufafanua kuwa TRC haina wakala yeyote wa ukataji wa tiketi za SGR, na wala haijaingia makubaliano na mtu au taasisi yoyote kutoa huduma hiyo kwa niaba yake.
Shirika linatoa onyo kwa wale wote wanaojaribu ama kutaka kufanya vitendo vya kughushi tiketi za SGR, kuwa ni kinyume cha Sheria ya kanuni za adhabu sura namba 16 marejeo ya 2002 kifungu 333 mpaka 335 vinavyokataza udanganyifu kupitia nyaraka, ambapo mojawapo ni vitendo vya kughushi.
Aidha Sheria namba 10 ya Reli ya mwaka 2017 kifungu cha 87, kinasema mtu yoyote atakayejipatia tiketi ya Shirika la Reli kwa kwa udanganyifu, atakuwa ametenda kosa na adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka miwili au faini isiyopungua milioni 5 na isiyozidi shilingi milioni 10 ama vyote kwa pamoja.
Kwa mantiki hiyo, Shirika linatoa wito kwa wananchi wote kuhakikisha wanakata tiketi kupitia njia rasmi pekee ambazo ni:
✅ Kupitia kiunganishi rasmi: sgrticket.trc.co.tz
✅ Au kufika moja kwa moja katika stesheni zetu zote za SGR na kukata tiketi dirishani.
Kwa taarifa zaidi au msaada, wasiliana nasi bure kupitia kituo cha huduma kwa wateja nambari 0800110042 ama kupitia WhatsApp nambari 0738 594 962 na mitandao yetu rasmi ya kijamii.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni