Breaking


Jumamosi, 9 Agosti 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI: PSG WANATARAJIA OFA KWA AJILI YA DONNARUMMA

 

Paris St-Germain wanatarajia ofa kutoka kwa Chelsea, Manchester United au Inter Milan kwa ajili ya mlinda lango wa Italia Gianluigi Donnarumma, 26. (ESPN)

Newcastle wanajipanga kuwasilisha ofa ya pauni milioni 30 kumnunua mshambuliaji wa Brentford mwenye umri wa miaka 28 kutoka DR Congo Yoane Wissa. (Times)

Newcastle wameanza mazungumzo na PSG kuhusu mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 26. (Florian Plettenberg)

Hakuna maoni: