Breaking


Jumatatu, 25 Agosti 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU: LIVERPOOL KURUDI NA DAU JIPYA KWA ISAK WIKI HII


 Liverpool wamepangwa kuwasilisha dau jipya kwa ajili ya Alexander Isak baada ya dili yao ya awali ya £110 m (plus add-ons) kukataliwa na Newcastle. 

 

Iwapo Liverpool wataongeza gharama hadi karibu £130 m, kuwepo na uwezekano mkubwa deal itakamilika  hasa pale Newcastle watakapopata mbadala. 

 Hadi sasa, Newcastle wamekuwa wakisema Isak hatakiwi kuuzwa, wakimnukuu kuwa bado hajabadilika msimamo na ni sehemu ya timu  lakini hisia ya kuachana (preference) inaongezeka. 

 Meneja wa Liverpool, Arne Slot, ameeleza kuwa, ingawa wanamchukulia Isak kama kipaumbele, anaweza kusaidia timu pia kwa wachezaji kama Chiesa, Ekitike, Gakpo, na Wirtz  akionyesha kwamba timu ina “kushikilia” hata bila Isak. 

Mbali na Isak, Liverpool pia wanaangalia mbadala kama Rodrygo wa Real Madrid, endapo manunuzi ya deal ya forward haifanyiki. 

Winga wa Manchester City, Savinho, bado ndiye chaguo namba moja la Tottenham, ambapo kocha Thomas Frank anataka kumsajili nyota huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 21 baada ya Spurs kumkosa Eberechi Eze, 27, aliyehamia Arsenal (Independent).

Tottenham wameweka wazi kwa Manchester City kuwa wako tayari kulipa pauni milioni 60.7 kumpata Savinho, ambaye naye anatamani kujiunga na klabu hiyo ya London (Talksport).

Katika juhudi za kufanya usajili mzuri, Tottenham pia wamewasilisha ofa iliyoboreshwa ya pauni milioni 43 kwa ajili ya kiungo wa Como na Argentina, Nico Paz mwenye umri wa miaka 20, lakini klabu hiyo ya Italia inashikilia msimamo wa kutaka dau la karibu pauni milioni 60 (Sky Sports Italia).

Manchester City, Arsenal na Liverpool zote zinaonyesha nia ya kumsajili winga wa Real Madrid na Brazil, Rodrygo, mwenye umri wa miaka 24, lakini hadi sasa klabu hiyo ya Uhispania haijapokea ofa yoyote rasmi kutoka kwa timu hizo (Marca).


Hakuna maoni: