Breaking


Jumatatu, 11 Agosti 2025

TLP YAJA NA VIPAUMBELE VITATU

MGOMBEA wa Chama Cha Tanzania Labour Party(TLP),Yustas Rwamugira,amechukua fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya urais na kutaja vipaumbele vitatu watakavyovisimamia ambavyo ni ulinzi na usalama,utawala bora na uchumi imara.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 11,2025,Yustas ameambatana na mgombea mwenza wa chama hicho Amana Suleiman Mzee,amesema cha kwanza ni nchi itawalike na iwe salama.

"Kipaumbele chetu cha kwanza nchi itawalike,iwe salama na katika uchaguzi huu tutaufanya kwa amani,la pili kila kitu ni lazima kiende kwa utaratibu kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi,utawala bora ndio utawafanya wafanye kazi vizuri na kujenga uchumi imara,"amesema.

Hakuna maoni: