Rais wa Marekani, Donald Trump, ametishia kuchukua hatua kali dhidi ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin ikiwa hatokubali kumaliza vita nchini Ukraine.
Rais Trump amesema Putin anapaswa kujiandaa kwa hilo, ikiwa mazungumzo kati yao katika mkutano uliopangwa kufanyika kesho katika jimbo la Alaska, hayatozaa matunda.
Kiongozi huyo wa Marekani kwa mara nyingine amependekeza kuhusu uwezekano wa kuwakutanisha Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky na Putin, mara baada ya mazungumzo ya Alaska.
Hata hivyo, amesema anasubiri kuona jinsi mkutano wake na Rais Putin utakavyomalizika, kwani huenda kusiwe na mkutano mwingine.
Rais Trump anapanga kukutana na Putin jimboni Alaska nchini Marekani, kutafuta suluhu ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine ambavyo vimedumu kwa takriban miaka mitatu na nusu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni