Breaking


Ijumaa, 29 Agosti 2025

TUPO TAYARI NA TIMAMU KUITANGAZA ILANI YA CCM


 Mgombea Mwenza kupitia Chama cha Mapinduzi Balozi Dokta Emmanuel Nchimbi amewasili Jijini Mwanza tayari kuanza kampeni katika kanda ya Ziwa. 

Dokta Nchimbi  amepokelewa na viongozi mbalimbali wa mkoa katika uwanja wa ndege wa Jijini Mwanza. 

Mara baada ya kuwasili Dokta Nchimbi amesema ameshukukuru kwa mapokezi makubwa yeye timu yake aliyopata tayari kwa ajili ya kuitangaza ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025 - 2030. 

Dokta Nchimbi amesema wapo timamu na tayari kuipeperusha bendera ya CCM ili kukipatia ushindi chama. 

Leo Dokta Nchimbi atafanya mkutano mkubwa katika Uwanja wa furahisha Jijini Mwanza

Hakuna maoni: