Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Tume ya Mipango na wadau mbalimbali wa maendeleo, limewahimiza wanahabari kushiriki kikamilifu katika kufanikisha Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 (TDV 2050).
Wito huo umetolewa na Bi. Melissa McNeil-Barrett, Naibu Mwakilishi na Kaimu Mkuu wa UNFPA nchini Tanzania, katika warsha ya waandishi wa habari iliyoandaliwa kwa ajili ya kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika utekelezaji wa Dira hiyo.
Bi. McNeil-Barrett amesema kuwa TDV 2050 inalenga kuboresha afya, elimu, na ushiriki wa vijana katika maamuzi yanayohusu maisha yao, huku ikijikita katika misingi ya usawa, ubunifu, maendeleo ya rasilimali watu na utunzaji wa mazingira.
Ameeleza kuwa mafanikio ya Dira hiyo yanategemea ushiriki wa wananchi wote na uelewa wa pamoja juu ya malengo yake.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni