Breaking


Jumatatu, 4 Agosti 2025

WAANDISHI EPUKENI HABARI ZA UCHOCHEZI-INEC

Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC, imewataka waandishi wa habari nchini katika kipindi hiki cha kuelekea, wakati na baada ya uchaguzi mkuu, kuepuka kuandika habari za uchochezi au zinazosababisha vurugu katika nchi.

Kauli hiyo ya INEC imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi INEC KAILIMA RAMADHAN, alipokua akizungumza katika mafunzo ya Wahariri na Waandishi wa habari yaliyoandaliwa na Tume hiyo.

KAILIMA amefafanua waandishi wanatakiwa kuripoti taarifa za uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani kwa usahihi na maudhui yake yalenge kuongeza Amani na mshikamano wa Kitaifa.



Hakuna maoni: