KAMISHNA wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt.Baghayo Saqware amesema, wanufaika wa huduma za bima nchini wameongezeka kutoka milioni 14 mwaka 2021 hadi milioni 25.9,mwaka huu huku hamasa ikiendelea ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika.
Dkt. Saqware ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi kati ya wahariri na waandishi wa habari nchini chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).
Pia, amesema mali na mitaji katika soko la bima imeongezeka kutoka shilingi trilioni 1.2 mwaka 2021 hadi trilioni 2.3, mwaka huu.
Ameongeza Amesema, pia mafanikio hayo yanatokana na hamasa na elimu inayotolewa na mamlaka kupitia mifumo mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari nchini.
Katika hatua nyingine, amesema wamefanikiwa kuimarishwa kwa mifumo ya TEHAMA kutokana na maelekezo ya Rais Dkt. Samia ambapo mamlaka imepiga hatua kubwa na imeweza kuunganisha mfumo wake na Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Mapato Tanzania, LATRA, TASAC na NIDA.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw.Sabato Kosuri amesema kuwa, ustawi wa taasisi za umma unategemea mahusiano mazuri na vyombo vya habari, kwani ni daraja muhimu katika kuunganisha umma.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni