Breaking


Jumatano, 27 Agosti 2025

YANGA PRINCESS WANASHUSHA BUSTA

Ni kama Yanga Princess wamepania kurejesha heshima yao kunako Ligi Kuu Soka ya Wanawake msimu ujao wa 2025-26, baada ya hivi punde kutangaza kuwa wamemalizana na Kiungo fundi Riticia Nabbosa kutokea Simba Queens.

Ikumbukwe pia Yanga Princess tayari walianza kuibomoa Simba Queens mapema tu kwa kumg'oa Precious Cristopher akiwa mchezaji huru huku Ritcia Staa wa pili kutoka Simba Queens kutua Yanga. Pia tayari walimuongeza Ogbonna Akudo huku wakiwabakiza Diana Mnally, Angel Michael, Uzoamaka Igwe na Akare Korrita.

Msimu ujao wanaume balaa na wanawake balaa.🔥

Hakuna maoni: