Breaking


Alhamisi, 4 Septemba 2025

CCM NI MWALIMU WA ILANI KWA NCHI ZINGINE

 

Mgombea Mwenza wa Urais Kupitia Chama cha Mapinduzi Balozi Dokta Emmanuel Nchimbi amesema zipo nchi ambazo zimekua zikiomba kufundishwa na CCM namna gani kinafanya kufanikiwa katika utekelezaji wa Ilani yake.

Dokta Nchimbi amesema hayo Septemba 03, 2025 katika mkutano wa kampeni uliofanyika shinyanga mjini.

Amesema ilani ya CCM imetekelezwa kwa viwango vya juu ambavyo havijawahi kutokea na hivyo kufanya baadhi ya mataifa kutaka kuja kujifunza.

Mgombea Mwenza Dokta Nchimbi amesema siri ya mafanikio hayo ya utekelezaji ni kwa sababu CCM ni chama shirikishi kinacho washirikisha wananchi kwa kujua agenda zao na mahitaji yao.

Amesema Serikali ya CCM imekua ikifanyakazi kubwa ya kutafuta fedha na kushusha chini katika utekelezaji wa ilani kwa kushirikiana na wananchi ambapo amewataka watanzania kutembea kifua mbele akijivunia Chama cha ukombozi.

Hakuna maoni: