Breaking


Jumatatu, 15 Septemba 2025

KAMPENI ZA CCM ZAANZA KWA KISHINDO PEMBA, MAELFU WAJITOKEZA.


Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimezinduliwa kwa kishindo kisiwani Pemba katika viwanja vya Gombani ya Kale, zikihudhuriwa na viongozi waandamizi wa chama na serikali.

Miongoni mwa viongozi walioshiriki ni Mgombea Urais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Makamo wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdullah pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa.

Maelfu ya wananchi walijitokeza kwa wingi, wakiwa wamevalia mavazi ya kijani na njano, ishara ya mshikamano na uungwaji mkono kwa chama chao.

Hafla hiyo ya kihistoria iliambatana na burudani na shamrashamra zilizowasha hamasa kubwa kwa wapenzi na wafuasi wa CCM kisiwani humo.


Uzinduzi huu umetajwa kuwa mwanzo wa safari yenye nguvu kwa chama hicho kuelekea uchaguzi ujao, huku viongozi wakisisitiza mshikamano na umoja kwa Wazanzibar.

Hakuna maoni: