Breaking


Ijumaa, 24 Aprili 2026

JUKWAA LA WANAWAKE VIONGOZI (WLF) LATANGAZA KUJITAMBULISHA RASMI

Jukwaa la wanawake viongozi nchini Tanzania, Women in Leadership Forum (WLF), leo Aprili 24, 2026 limetangaza rasmi kujitambulisha kwake, likiwa na lengo la kuimarisha sauti ya wanawake katika uongozi pamoja na kukuza mshikamano na mchango wao katika maendeleo ya taifa. Taasisi hiyo imeeleza kuwa uzinduzi wake rasmi utafanyika hivi karibuni, ukiwa sehemu ya juhudi za kuwaunganisha wanawake wenye ndoto na uwezo wa kuongoza katika ngazi mbalimbali.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mwenyekiti wa WLF, Dkt. Evelyne Munisi ambaye pia ni Mbunge, amesema jukwaa hilo linalenga kuonesha dhamira na mitazamo ya wanawake katika uongozi, huku likipanua wigo wa ushawishi wao ndani ya nchi na nje ya mipaka ya Tanzania. Amebainisha kuwa kupitia WLF, wanawake watapata fursa ya kushirikiana, kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo katika masuala ya uongozi.

Dkt. Munisi ameongeza kuwa jukwaa hilo linaundwa na wanawake waliowahi kugombea nafasi za juu za uongozi, zikiwemo urais na umakamu wa rais kupitia vyama mbalimbali vya siasa nchini. Amesisitiza kuwa uzoefu huo utasaidia kuwahamasisha wanawake wengine kujitokeza kwa ujasiri kushiriki katika uongozi na kuchangia kwa maendeleo ya taifa kwa mtazamo chanya na endelevu. 

Hakuna maoni: