Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asharose Migiro amepokea salamu za upendo kutoka kwa maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi Mbinga Mjini mkoani Ruvuma kwa ajili ya kumsubiria, kumlaki na kumsikiliza Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 leo tarehe 21 Septemba 2025.
Wananchi hao wameonesha shangwe na furaha yao kwa Katibu Mkuu na kumpa salamu zao za upendo wao wa dhati kwa Rais Dkt. Samia huku wakisema kuwa leo watampa maua yake ya kijani na njano kama ishara ya kumpitisha kwao bila kupingwa.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni