Breaking


Jumamosi, 13 Septemba 2025

KIGOMA NITATEKELEZA MIRADI YA KITAIFA- RAIS SAMIA


 MGOMBEA wa kiti cha rais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan,amesema endapo akipata ridhaa ya kushika dola atatekeleza miradi ya kitaifa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR na kukufua mradi wa kufua umeme katika Mto Malagalasi.

Miradi hiyo itaifanya Mkoa wa Kigoma kuwa lango la biashara ya kimataifa na kuchochea na kuvutia wawekezaji kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo viwanda.

Rais Samia amesema hayo Septemba 13,2025,katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kasulu Mjini.


"Tuna mradi wa kitaifa wa ujenzi wa reli ya  kisasa ya SGR  inayotoka Dar es Salaam hadi Kigoma ikifika Uvinza inakwenda mpaka Msongati nchini Burundi na Burundi wataijenga hadi Afrika Kusini,"


Amesema wamefanya hivyo ili waweze kufungua njia za kufanyabiashara, hivyo kuwaomba wakazi wa Kigoma kutumia fursa hiyo vizuri.

Hakuna maoni: