Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtumba kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Anthony Mavunde ameendelea na awamu ya kwanza ya kampeni yake ya mtaa kwa mtaa kwa kila kata kwa kuzungumza na makundi mbali katika Kata ya Kiwanja cha Ndege.
Akiwa kwenye mkutano huo Septemba 14,2025,amezungumza na wananchi wa Mitaa ya Oysterbay,Mkwajuni-Mailimbili, Mipango,Makongoro na Kiwanja cha Ndege(AREA C),na kuwaomba kujitokeza kupiga kura Octoba 19,2025.
Amesema siku hiyo ikifika kura zote za ndio ziende kwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Udiwani wa kata ya Kiwanja cha Ndefe Yonah Lekele,ili kukamilisha mafiga matatu.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni