Kilele cha Mwananchi Day 2025 kimeacha historia mpya kwa mashabiki wa Yanga SC baada ya klabu hiyo kukabidhiwa hati rasmi ya ujenzi wa uwanja wa kisasa eneo la Jangwani, makao yake makuu.
Hati hiyo ilipokelewa na Rais wa Yanga SC kwa niaba ya uongozi, huku Serikali kupitia Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ikihakikisha dhamira yake ya kuendeleza michezo nchini.
Uwanja huo utajengwa kwa viwango vya kimataifa, utachochea vipaji vipya, kuongeza mapato na kuvutia mashindano ya kimataifa. Mashabiki waliolipuka kwa shangwe wamesema sasa ndoto ya muda mrefu ya klabu yao iko karibu kutimia.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni